Huwa nawauliza wagonjwa wangu swali hili, “Leo hii ukiambiwa usipoacha ulevi wa pombe, sigara
au wanawake, mwanao au mama yako anafariki! Hautaacha?”
Au kwanini ikitokea ukaambiwa una kansa ya mapafu na moja ya njia ya kuongeza maisha yako ni kuacha sigara, mbona wagonjwa wengi huwa wanaacha?
Au kwanini watu wakifiwa na ndugu zao na wakaamua kuokoka huwa wanaacha sigara na pombe bila kwenda hata rehab?
Fahamu mengi kuhusu majibu haya na mengineyo kupitia kitabu hiki.
Kuhusu
Mwandishi: Dr. Ansbert Mutashobya
Mhariri: LEO Kidijitali
Mchapishaji: Abite Medical and Health Services Ltd.
Ansbert Mutashobya –
Kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili yako wewe unayeteseka na ulevi.
Ulevi wowote ule ni adui wa afya na maendeleo kwa ujumla.
Hakuna Mtu anayependa kuwa mlevi bali hujikuta tu umetumbukia huko.
Swali ni Je! Umeshatumbukia kwenye ulevi na kiuhalisia afya yako na ndoto zako zinamomonyoka taratibu.
Utatokaje?
Kitabu hiki kina majibu ya kusaidia, njia hizi zilizoandikwa hapa zilinisaidia Mimi kuondokana na ulevi wa kunywa kokakola.
Enjoy!